Kupoteza kumbukumbu ni ugonjwa unaoingia kwa kasi ugonjwa Umetajwa sasa unakuja juu kuliko maradhi sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na saratani Kupoteza kumbukumbu hutokea pale eneo la ubongo linalohusika katika kuhifadhi taarifa linapoathirika. Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa kawaida unawapata wazee. Uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1906 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili, Alois Alzheimer. Dk Alzheimer, ambaye ni MjerumU ani, alipata mgonjwa mwenye tatizo hilo ambaye alikuwa anapoteza kumbukumbu, kuchanganyikiwa na kupata ugumu wa kuelewa maswali anayoulizwa. Mgonjwa huyo alifariki dunia na ndipo Dk Alzheimer alipofanya uchunguzi katika ubongo wa marehemu na kubaini kuwa kulikuwa na hitilafu katika baadhi ya seli za ubongo wake. Hivyo, akawa daktari wa kwanza kubaini ugonjwa huo wa kupoteza kumbukumbu na kulifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) limpe heshima kwa kuuita ugonjwa huo jina la daktari huyo. Ugonjwa huo unafahamika kama ...