Skip to main content

Wanafunzi Darasa la Saba waliofaulu Wapangiwa Shule Wote.

Baada ya kupata ufaulu mzuri na kuongoza kitaifa katika matokeo ya Darasa la saba mkoa wa Dar es Salaam,leo umetangangaza kuwa hakutakuwepo na wanafunzi wa chaguo la pili badala yake wanafunzi wote wamepangiwa shule moja kwa moja. Akizungumza katika Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2017 wa mkoa huo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando amesema kuwa katika matokeo ya Darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 58,573 walifanya sawa na asilimia 100% wote wamepangiwa shule na Wataanza kidato cha kwanza January 2018. Amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za ufaulu mzuri zaidi ni 68, wavulana 35 na wasichana 33. Wanafunzi walio walio chaguzi wa shule za ufundi ni 74,wavulana 68na wasichana 6,shule za bweni kawaida no 24wavulana 12 na wasichana 12. Aidha amesema, wanafunzi 1,931wamechaguliwa kujiunga na shule za mkoa zinazo chukua wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wavulana ni 850 na wasichana 1, 081. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule za serikali za wananchi ni 56,299 ikiwemo wavulana 27,035 na wasichana 29,264 huku wanafunzi wenye uhitaji maalum waliopangiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ni 101wavulana wakiwa ni 58na wasichana 43. Amefafanua kuwa, waliochaguliwa Manispaa ya Ilala ni wanafunzi 19,236,kigamboni 2,803,Kinondon 10,885 Temeke15, 323na Ubungo ni 10,326. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo Jumla ya nafasi 4,685 katika shule za pembenizomwajiji zimebaki wazi kwa sababu ya umbali uliopo kati ya shule ya msingi waliposoma wanafunzi na mahali shule zilipo, nafasi zizo baki kwa Manispaa ya Ilala ya Ilala (mjini) ni 887,kigamboni590, Kinondon 1,718 na Ubungo 1,490. Akizungumzia asilimia, amesema wanafunzi waliojiunga na shule za secondari kwa waliofanya mtihani kwa mkoa ni asilimia 87.82%. katika Manispaa ya Ilala (mjini) ni asilimia 92.48.Ilala (Vijijini) asilimia 84.42.Manispaa ya Kinondoni 93.02%Temeke 81.74%.Kigamboni 91.10% na Ubungo ni 89.01. Pamoja na hayo Mbando amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuwa peleka watoto wao shuleni waliopangiwa tarehe 8 January 2018bila kukosa, na kuwakumbusha wakuu wa shule 147 zinazo pokea wanafunzi kuzingatia waraka no 2 wa 2016 unao husu uendeshaji wa elimu bure bila malipo.

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...