Baada ya kupata ufaulu mzuri na kuongoza kitaifa katika matokeo ya Darasa la saba mkoa wa Dar es Salaam,leo umetangangaza kuwa hakutakuwepo na wanafunzi wa chaguo la pili badala yake wanafunzi wote wamepangiwa shule moja kwa moja. Akizungumza katika Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2017 wa mkoa huo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando amesema kuwa katika matokeo ya Darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 58,573 walifanya sawa na asilimia 100% wote wamepangiwa shule na Wataanza kidato cha kwanza January 2018. Amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za ufaulu mzuri zaidi ni 68, wavulana 35 na wasichana 33. Wanafunzi walio walio chaguzi wa shule za ufundi ni 74,wavulana 68na wasichana 6,shule za bweni kawaida no 24wavulana 12 na wasichana 12. Aidha amesema, wanafunzi 1,931wamechaguliwa kujiunga na shule za mkoa zinazo chukua wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wavulana ni 850 na wasichana 1, ...
THE FREEDOM OF CHOICE