Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na umeng’enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng’enyaji huo ni kinywa, umio/esofagasi (ujia wa msuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo), mfuko wa tumbo, ini, mfuko wa nyongo, duodenamu (sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo inayoanzia katika pilorasi ya tumbo). Nyingine ni iliamu (utumbo mdogo kati ya jejunamu na sikamu), kongosho, utumbo mpana na rektamu (sehemu ya mwishoni ya utumbo mkubwa yenye urefu wa sentimeta 13, rektamu huanzia mwishoni mwa koloni ya sigmoidi na kuishia mwanzoni mwa unyeo). Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng’enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama ‘Peptic Ulcers’. Vidonda vya mfumo wa umeng’anyaji chakula vikiw...