Skip to main content

FAHAMU KUHUSU KIFUA KIKUU (TUBERCULOSIS,TB)

MTU KWAO BLOG
@#Eagle eyes
Kifua kikuu ni ugonjwa unaosabishwa vimelea vidogo aina ya bakteria viitwavyo #Microbacteria_tuberculosis. Ugonjwa wa kifua kikuu unaenezwa kwa njia ya hewa kutoka katika mtu ambaye anaugua na hajaanza matibabu, mtu huyu akipiga chafya, kukohoa au kutema makohozi ovyo anaweza kuambukiza watu wengine.
Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, pia kinaweza kuathiri sehemu yeyote ile nyingine ya mwili ikiwemo mifupa, tumbo na mgongo.
VITU VINAVYOHATARISHA MTU KUUMWA KIFUA KIKUU(TB)
Zaidi ya theluthi moja ya watu duiniani wana maambukizi ya TB lakini hawana dalili za kifua kikuu, asilimia 10 tu ndio huja kupata ugonjwa wa kifua kikuu. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili huwa imara na kuzuia vijidudu vya TB kuzaliana na kushambulia mwili. Vitu vifuatavyo huchangia kwa namna moja au nyingine kutokea kwa kifua kikuu kwa mtu asiye na maambukizi:
    *UKIMWI/VVU
   * Upungufu wa kinga mwilini kutokana na dawa au magonjwa mengine ukiacha UKIMWI.
   * Kisukari
    *Utapiamlo
   * Uvutaji wa sigara
   * Unywaji wa pombe kupitan kiasi
#DALILI
Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kukohoa kwa wiki mbili au zaidi mfululizo, homa za mara kwa mara kwa wiki mbili au zaidi, kutokwa na jasho jingi hasa nyakati za usiku, kukohoa makohozi yenye damu, kupungua uzito zaidi ya kilo 3 ndani ya wiki 4 au kukonda pamoja na kukosa hamu ya kula.
Kifua kikuu hugundulika kwa kupima makohozi na ikibidi x-ray na matibabu yake ni bure katika hospitali zote za serikali na binafsi. Unapoona mtu ana dalili mojawapo kati ya hizi au wewe mwenyewe mshauri awahi kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba kwani mtu mmoja huweza kuwaambukiza watu kati ya 10 hadi 15 kwa mwaka kama hajapata matibabu
Wastani wa watu 176 huugua kifua kikuu kila siku nchini Tanzania na wastani wa watu 12 hufariki dunia kila siku .
Ikitokea umegundulika kuwa una kifua kikuu usihofu kwani kinatibika na mamilioni ya watu duniani kote wameugua na kupona. Unachotakiwa kufanya ni kufuata masharti utakayopewa na daktari kama; kunywa dawa kila siku kwa muda uliopangiwa ili kupona kabisa. Matibabu yake huchukua kati ya miezi sita hadi minane.
Endapo umegundulika kuwa na kifua kikuu kumbuka kufunika mdomo na pua unapo kohoa au kupiga chafya, ili usiambukize watu wengine na pia usiteme mate ovyo
.
Pumzika kiasi cha kutosha mahali penye hewa safi ya kutosha, kula chakula bora na uwafahamishe ndugu na marafiki kwamba unaugua kifua kikuu na uko kwenye matibabu, na ukisha kamilisha matibabu nenda kwa mhudumu wa afya kwa uchunguzi ili kuthibitisha kama umepona.
#Kumbuka ni muhimu kuendelea kutumia dawa mpaka mwisho hata kama unajisikia vizuri ili usipate kifua kikuu sugu ambacho matibabu yake ni magumu. Mara wa mara kifua kikuu kimekuwa kikihusishwa na ugonjwa wa ukimwi kwani asilimia 50 ya watu wenye kifua kikuu wana VVU. Kama umethibitika una kifua kikuu ni muhimu kupata ushauri nasaha na kupima virusi vya UKIMWI, kwani asilimia 10-15 ya watu wanaoishi na VVU wanaugua kifua kikuu, hivyo ni muhimu kuchunguzwa kama una kifua kikuu ili kuboresha na kuokoa maisha yako kwani kifua kikuu kinatibika kabisa hata kama una maambukizi ya VVU.
NB; TB ni ugonjwa unaotibika ikiwa upo katika hatua za awali ,hivo unashauriwa kufika kituo cha afya/hospitali mara moja unapohisi una Dalili za ugonjwa huu.
#AFYAniUHAI

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...