Hospitali ya taifa ya Muhimbili MNH Nchini Tanzania imesema kuwa huduma ya vipimo kwa wagonjwa imeimarishwa na kufanikiwa kuongeza wagonjwa waliopimwa kutoka 32,010 wa mwaka 2014/15 hadi kufikia 41,101 kwa mwaka 2015/16

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa wateja Aminiel Aligaesha imeonyesha kuwa mashine za MRI na CT-Scan zinafanya kazi vizuri na hakuna mashine mbovu inayosababisha msongamano wa wagonjwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa mashine hizo ziklisimama kwa siku moja mpaka mbili katika mwezi wa juni ili kupisha matengenezo hivi sasa hali imeimarika na huduma zinaendelea kama kawaida.
Comments
Post a Comment