Skip to main content

IJUE HOMA YA MANJANO HAPA


MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes
CHANZO, ATHARI  , KINGA   NA  TIBA  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano    ambao  hufahamika  kitaalamu  kama  HEPATITIS  B  ni  hatari  sana  na  umesababisha  vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote.    Kwa  mujibu  wa  ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  ( W.H.O )   kuna  zaidi  ya  wau  Milioni  350  duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu  hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa  kila  mwaka  kwa  ugonjwa  wa  Manjano.
CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (  HBV )  ambavyo  hushambulia    zaidi ini  la  mwanadamu.   Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza  uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  asratani  ya  ini  ambayo  hupelekea  kifo.
MAMBO  YASABABISHAYO  MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :
i.   Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
ii. Kunyonyana  ndimi
iii. Kuchangia  damu  isiyo  salama
iv. Mama  mjamzito mwenye  ugonjwa  huu  anaweza  kumuambukiza  mtoto  wake  wakati  wa  kujifungua.
v. Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na  sindano.
DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu  kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza  kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa  kiwango  kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama  ifuatavyo :
i.  Uchovu  wa  mwili
ii. Kichefuchefu
iii. Mwili  kuwa  dhaifu
iv. Homa  kali
v.  Kupoteza  hamu  ya  kula
vi. Kupungua  uzito
vii. Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
viii. Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
ix. Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.
KINGA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
i.  Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya  ugonjwa  huu.
ii. Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
iii. Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
iv. Kutochangia  mswaki
v.  Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
vi. Kuto ongezewa damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika  kuwa  salama.
TIBA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi  hospitali  atapatiwa  dawa za  kupambana  na  virusi  kuvipunguza  nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini  lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu  kupata  ini  salama.
Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu  unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa  za  kulevya  na  vitu  vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi  wa  ini.

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...