Skip to main content

IMANI POTOFU KUHUSU AFYA YA KINYWA NA MENO


MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes
1.POTOFU: 
Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno
UKWELI: 
Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika, suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu kunaweza kupelekea kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika.
Kupiga mswaki marambili, taratibu na kwa njia sahihi ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya
2.POTOFU: 
Huna haja ya kumuona tabibu wamenokama hujaona au kuhisi una tatizo la meno.
UKWELI:
 Kila mtu anatakiwa kumuona tabibu wa meno angalau mara mbili kwa mwaka bila kujali meno yake yanaonekana vizuri au imara kiasi gani.
Si meno yote yanayo onekana mazuri na imara ni mazima, mengine yanaweza kuwa yameoza katikamaeneo usiyoweza ona kama chini ya fizi na kwenye mizizi, si hivyo tu hata uoto mpya(neoplasm)uweza kugundulika mapema kabla ya kufanya uaribifu mkubwa kama utachunguzwa na wataalamu.
Kumbuka pia mangonjwa ya mifumo mingine kama ukimwi,kisukari na mengine mengi hujidhihirisha mapema kinywani kabla mgonjwa hajapata dalili zingine.
3.POTIFU:
Usile kitu chochote unapo kwenda kung’oa jino
UKWELI:
Njaa inaweza kukufanya uzirahi katika zoezi la kungoa jino, hofu ikichanganyika na sukari kidogo mwilini husababisha ubongo kushindwa kufanya kazi sawa sawa.
Imani hii potofu inahusishwa na sindano ya ganzi, watu wengi wanafikiri kila ganzi inatakiwa mtu awe hakula kwa muda fulani.
Hii kwa matibabu ya meno sio kweli kwani ganzi hutolewa kwenye eneo husika tu(local anaesthesia)hivyo haiathili mwili mzima.
4.POTOFU:
Usitoe jino au kufanya matibabu ya mzizi wa jino kama una uvimbe hasa usaha
UKWELI:
Kung’oa jino au matibabu ya mzizi wa jino yanasaidia kutoa nafasi/njia kwa usaha kutoka na hivyo kupona haraka pengine bila hata kuhitaji dawa(antibiotics).Yaweza kuwa kweli pale tu kama mgonjwa atukuwa na homa au hawezi fungua kinywa ambapo itabidi udhibiti homa kwanza, na kama ni kushindwa kufungua kinywa yabidi kuacha na kutibu kinacho mfanya ashindwe kufungua kinywa kwanza.
5.POTOFU:
Mama mjamzito hastahili kutoa jino mpaka atakapo jifungua
UKWELI:
Kumuacha mama mjamzito na maumivu pamoja na ugonjwa kwaweza kufanya ugonjwa kusambaa na kuingia kwenye ubongo hata kupelekea kifo cha mama na kiumbe chake. Pia maumivu makali yaweza kusababisha mimba kutoka.
6.POTOFU:
Njia ya uhakika ya kutibu jino ni kuling’oa
UKWELI:
Ziko njia nyingi na za uhakika za kutibu jino bila kungoa. Kung’oa jino kama tiba ni pale tu ambapo jino hilo haliwezi tibika kwa njia yeyote na kukaa kwake kwa weza kuleta madhara zaidi.
Kutoa jino huleta madhara mengine na meno bandia pamoja na kwamba hayawezi kurejesha kazi za meno yaliyotoka kwa kiwango halisi, lakini pia utunzaji wake ni mgumu na gharama pia. Hata hivyo kama umelazimika kupoteza meno basi meno bandia ndilo chaguo pekee.
7.POTOFU:
Kuweka dawa ya kutuliza maumivu kama aspirini kwenye tobo kunasaidia kutoa maumivu.
UKWELI:
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, kutuliza maumivu wakati kisababishi cha maumivu hakija shugulikiwa ni kulikuza tatizo kwa gharama.Mbali na hivyo dawa kama aspirini uunguza fizi zilizozunguka jino ulimoiweka, pia ulilainisha(weaken)na kufanya uotaji wake uwe mgumu kwani uvunjika vunjika hovyo hovyo
8.POTOFU:
Kutoa jino husababisha kifo
UKWELI:
Kuendelea kukaa na jino lililooza na halifai kuzibwa hufanya ugonjwa kusambaa na kusababisha kifo. Unaonekana kama ukweli pale tu mgonjwa anakuja hospitalini kutoa jino
9.POTOFU:
Meno mazuri urithishwa(inherited)
UKWELI: 
Eti kwa vile tu mama au baba ana meno mazuri na mazima na wewe utakuwa hivyo au kinyume chake.
Urithi unachangia kiasi kidogo sana, utunzaji wa meno vizuri na kukutana na tabibu wa meno mara kwara ndio njia muhimu ya kuweka meno na kinywa chako sawa.
10.POTOFU: 
Hakuna haja ya kuhangaika na meno ya utotoni kwani yatatoka baada ya muda wake kufika
UKWELI: 
Meno ya utotoni yasipotunzwa vizuri yanaweza kusababisha kutoka/ kutolewa kabla ya muda wake na kupelekea meno ya ukubwani kuota kwa mpangilio usiopendeza, lakini pia katika kipindi cha mchanganyiko wa meno ya ukubwani na utotoni, meno ya utotoni yaliyooza yaweza ambukiza ya ukubwani.
11.POTOFU: 
Maumivu ya meno yatajiishia yenyewe baada ya muda.
UKWELI:
Kama jino limeoza haliwezi pona kwa namna yoyote mpaka lipate tiba hata kama haliumi. Ukiendelea kulidharau ugonjwa unaweza kusambaa mpaka maeneo mengine kama ubongo, kifuani na hatimaye kusababisha kifo.
Angalizo: 
Ni asilimia tano tu kati ya wagonjwa ambao tatizo la jino limesambaa hadi kwenye ubongo ndio huweza kupona..

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...