UFAULU KIDATO CHA SITA ULAYAS SECONDARY WILAYANI LUDEWA WASHUKA
Mwl. Timoth Haule Mwalimu mwandamizi Taaluma Ulayas Secondary Ludewa
Mwl. Phoady Ngoloka mwalimu wa Nidhamu Ulayas Secondary Ludewa Na Maiko Luoga Ludewa. Shule ya Sekodari Ulayasi Iliyopo katika kata ya Mlangali wilayani ludewa katika Mkoa Wa Njombe yenye Kidato cha kwanza hadi cha sita Imekuwa ikisifika kwa Umahiri wake Wa Kufaulisha zaidi wanafunzi na kupokea wanafunzi kutoka Maeneo Tofauti ya Nchi lakini Hivi karibuni Shule hiyo imeripotiwa kufanya vibaya Kwa upande Wa Taaluma sababu kubwa ikiwa ni Ubovu Wa nidhamu kwa wanafunzi Wa Shule hiyo. Siku chache baada ya Serikali Kutangaza Matokeo ya Kidato cha sita nchini Kwa mwaka huu 2016 Nimefika katika Shule ya Secondary Ulayasi Iliyopo Eneo la Mlangali ndani Wilayani Ludewa Nakuzungumza na Baadhi ya walimu Akiwemo Mkuu Wa Shule hiyo Mwalimu Hashimu Masoli Ambaye ameyaweka Bayana matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2016 katika Shule yake ya Secondary Ulayasi ambapo yanaonesha kuwa Division One zipo 10, Division Two zipo 53, Division Three Zipo 72 Huku Division For zikiwa 11 na Division Zero ni 3. Hatahivyo Mwalimu huyo Ameongeza kuwa Shule yake imeshika nafasi ya pili Kiwilaya Kati Ya shule mbili za A -Level zilizopo wilayani Ludewa Huku ikishika Nafasi ya 11 Kimkoa kati ya shule 11 za mkoa Wa Njombe na Kitaifa Shule hiyo ni ya 312 kati Ya Shule 423 Hivyo matokeo hayo yameifanya shule ya Secondary Ulayasi Kushuka Kitaaluma kwa Mwaka huu Ukilinganisha na Mwaka 2015 Ambapo Mwalimu Masoli amesema Hiyo imesababishwa na Tabia mbaya waliyokuwa nayo Baadhi ya wanafunzi ya Kufanya vurugu Mwaka 2015 Wakati Shule hiyo ikisimamiwa na Mwalimu Mkuu mwingine tofauti na yeye. Mwalimu Phoady Ngoloka Ni Mwalimu Wa Nidhamu Katika Shule ya Ulayasi Secondary Amesema kuwa Hapo mwanzo Wanafunzi Wa shule hiyo walikuwa hawana nidhamu Bora Hali iliyosababisha Shule hiyo kufanya Vibaya katika Matokeo ya Kidato cha Sita Mwaka huu 2016 Hivyo mara baada ya Kulibaini tatizo hilo wao Kama Bodi ya Shule wamepanga Kuimarisha Nidhamu kwa wanafunzi ili kuweza kutoa matokeo Mazuri ya Kidato cha sita ifikapo mwaka 2017 na Kurudisha Hadhi ya Ulayas Secondary iliyotawala Miaka Mingi iliyopita. Naye mwalimu Mwandamizi Wa Taaluma katika Shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Thimoth HauleAmekiri kufanya Vibaya Katika Matokeo hayo ya kidato Cha Sita na kwamba Hayairidhishi jamii ya Watanzania Hivyo Wao wameliona Tatizo hilo na kuamua kujipanga katika kufundisha kwa bidii Na kumubana kila mwalimu Kuhakikisha anafundisha Vipindi vyake Kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na Kuongeza walimu wakujitolea ili waweze Kuziba Pengo la Walimu katika shule yao. Kwaupande wake Diwani Wa Kata Ya Mlangali ilipo Shule hiyo Mh. Khamis Kayombo amesema kuwa amefanya kikao na Mkuu Wa Shule hiyo na kumuagiza Kuanza kubadilika Maramoja katika utendaji kazi wao Huku akiwaaminisha wananchi Wa Tanzania kuwa Sasa Mkakati maalumu Umewekwa Hivyo waamini Shule
![]() |
Muonekano wa Jengo la Utawala Ulayas Secondary |
![]() |
Mwl. Masoli Mkuu wa SHule Ulayas Sekondary Ludewa |


🔥
ReplyDelete