Skip to main content

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE

 

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na umeng’enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali.

Sehemu kuu zinazohusika katika umeng’enyaji huo ni kinywa, umio/esofagasi (ujia wa msuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo), mfuko wa tumbo, ini, mfuko wa nyongo, duodenamu (sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo inayoanzia katika pilorasi ya tumbo).

Nyingine ni iliamu (utumbo mdogo kati ya jejunamu na sikamu), kongosho, utumbo mpana na rektamu (sehemu ya mwishoni ya utumbo mkubwa yenye urefu wa sentimeta 13, rektamu huanzia mwishoni mwa koloni ya sigmoidi na kuishia mwanzoni mwa unyeo).

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng’enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama ‘Peptic Ulcers’.

Vidonda vya mfumo wa umeng’anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo ‘Gastric Ulcer’, vikiwa katika duodenamu tunaita ‘Duodenal Ulcer’ na vikiwa katika esofagasi tunaita ‘Esophageal Ulcer’

Nini husababisha vidonda vya tumbo?
Kisababishi kikuu ni bakteria aina ya helicobacter pylori ni kupitia vyakula na maji. Pia, hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo kama wapenzi wanaonyonyana ndimi.

Bakteria hao huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng’enya viitwayo urease inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.

Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.

Sababu nyingine ni chembe za urithi genetics. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu na wenye vidonda pia. Hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.

Uvutaji sigara na tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo.

Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

Dalili za vidonda
Ieleweke ni mara chache mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili.

Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi; 


  • Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. 
  • Maumivu yanaweza kuanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua. 
  • Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia, yanaweza kuwa makali wakati wa usiku yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.


Dalili nyingine ni kushindwa kumeza vizuri chakula au kukwama kama kinataka kurudi mdomoni, kujisikia vibaya baada ya kula, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula.

Dalili hatari ni pamoja na kutapika damu, kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito na kupata kichefuchefu na kutapika.

Jinsi ya kugundua vidonda vya tumbo
Maelezo ya mgonjwa kuhusu dalili humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mgonjwa kuwa ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika. Kupima damu kuangalia bakteria aina ya h.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ mfano Omeprazole. Vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi.

Kupima pumzi. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya saa moja mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa. Ikiwa mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi. Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria h.pylori kwenye kinyesi. Vilevile kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

Kufanya x-ray ya sehemu ya juu ya tumbo ‘upper gastrointestinal x-ray’. Picha huonyesha ‘esophagus’, mfuko wa tumbo ‘stomach’ na dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye ‘Barium’ ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwenye x-ray.

Matibabu
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria h.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na ‘NSAIDs’ na hana maambukizi ya bakteria h.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole.

Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo ‘Proton Pump’ ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatarithiwa na dawa kama Paracetamol.

Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya ‘PPIs’ hazitokuwepo.

H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo ‘Histamine’ ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi, hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi ‘Antiacids’ & ‘Alginates’ kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...