Skip to main content

Mchungaji Afariki kwa Kufunga Siku 30 Akijaribu Kuvunja Rekodi ya Yesu


MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes
LILE andiko la usimjaribu bwana Mungu wako lililosemwa na Yesu Kristu limejidhihirisha baada ya mchungaji maarufu nchini Afrika Kusini, Alfred Ndlovu (44), kufariki dunia baada ya kufunga usiku na mchana kwa takribani siku 30 akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 bila kula kitu chochote.
Kama alivyofanya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu naye aliondoka nyumbani kwake Juni  17 mwaka huu na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka pembeni anasa za dunia.
Kifo cha mchungaji huyo kimeishangaza sana familia yake, waumini wa kanisa lake na jamii nzima kwa ujumla.
Mchungaji huyo alijulikana kwa imani yake thabiti ambayo  ingeweza hata kuhamisha milima.
Mmoja wa wanafamilia ya mchungaji huyo alisikika akilalamika; “Alikuwa mtu wa imani sana.
Lakini kwa bahati mbaya amefariki kifo hicho. Baada ya mwezi ndipo tumepata taarifa za kifo chake”
Akijaribu kuvunja rekodi ya Yesu, Mchungaji Ndlovu alifariki baada ya kufunga kwa takribani siku 30 japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa wowote hapo awali. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake iligunduliwa na mpita njia mmoja aliyetoa taarifa polisi.

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...