MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake tangu ashike nafasi ya urais Novemba mwaka jana. Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo wa zamani amebainisha kuwa ingekuwa ni yeye amepata nafasi ya urais, angeanza na vipaumbele vyake ambavyo ni ajira na maslahi ya walimu ili kuboresha zaidi maeneo hayo. Lowassa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na mtangazaji Tido Mhando kwenye kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Televisheni ya Azam. Alikiri kuwa Dk Magufuli hadi sasa ameonekana kufanya vizuri katika utendaji wake, ikiwemo suala la ufisadi na hatua yake ya kutekeleza kwa vitendo kuhamishia serikali mkoani Dodoma. “Amefanya kazi nzuri katika maeneo fulani, amefanya vizuri sana. Kuna maeneo amesema mwalimu unaweza kufagia shilingi, na yeye amefagia shilingi. Ila kuuna maeneo kwa maoni yangu ningeyapa kipaumbele zaidi kwa mfano ajira,” alisisitiza. ...
THE FREEDOM OF CHOICE