DC Aagiza Mganga Kusimamishwa Kazi Geita
MKUU wa wilaya Geita Hermani Kapufi , amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Geita Alli Kidwaka kumuondoa mara moja mganga wa Zahanati ya Karoro wilaya na mkoa wa Geita Daniel Zengo , kwa madai ya kuuza dawa za Serikali kwenye duka lake binafsi.
Amesema hayo wakati akizungumza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika kwenye Stand mjini Katoro lengo likiwa ni kujadili shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Kapufi amesema kuwa mganga huyo anatakiwa kuondoka kwenye kituo hicho na kufunga duka lake mara moja huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama kufuatilia.
Naye mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Geita amekili kuwepo kwa changamoto hizo na kuahidi kunza kuzitatua
Comments
Post a Comment