Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi
iliyotolewa leo July 28 2016 mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James
Munanka Wanyancha.
Rais Magufuli ametengua uteuzi huo
kuanzia leo July 28 2016. Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais
Magufuli amemteua Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko
wa Barabara.
Uteuzi wa
Joseph Odo Haule umeanza leo July 28 2016. Kabla ya uteuzi huo Joseph
Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund). Wajumbe
wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
Comments
Post a Comment