USHAURI KWA WANAFUNZI WANAOTARAJIA KUOMBA VYUO VIKUU KUPITIA TCU 2016/2017
Nachukua nafasi hii kuandika makala hii kuweza kutoa ushauri na kuweza kuwaeleza machache niyajuayo katika sakata zima la uombaji wa vyuo vikuu kupitia TCU. Uombaji wa chuo ni swala nyeti ambalo linahitaji umakini na ushaur chanya kuweza kukamilisha mchakato huo kikamilifu.Yafuatayo ni mambo ambayo unapaswa kuzingatia katika uchaguzi wa chuo na fani tahasusi.
1) MATOKEO YAKO NDIO KIGEZO CHAKO:
Jambo la msingi kabisa ni kujitathmini kua kutokana na matokeo yangu haya naweza kusomea fani gani,na chuo gani ili kuweza kufikisha malengo yangu.Katika nukta hii napenda nigusie vitu vifuatavyo kwa ufupi kabisa.
I. Kwanza,nikupitia vizuri muongozo wa kitabu cha TCU,Hapo utapata kuoana orodha ya vyuo tafauti ,fani ,minimum entry requirements pamoja na gharama ya chuo husika.
II. Kutafuta washauri na wataalamu ambao wanaweza kukushauri vizuri kuhusu vyuo unavotaka kuomba fani na mengineyo ya msingi.
III. Usifuate mkumbo katika kuomba chuo : hapa wengi huwaathiri huomba kwa kufuata rafiki yake kaomba vipi nayeye akafuata,ifahamike fika kua watu hutafautiana ki malengo,fikra lakini pia mnatafautiana pengine hata matokeo yenu,hivyo kwa hapa nitaendelea kusisitizia umuhim wa kupata washauri wazuri .
2) UPANGAJI WA FANI NA CHUO HUSIKA KULINGANA NA PRIORITY
Hii ni moja kati ya nukta muhimu sana ambayo inahitaji umakini mkubwa katika mchakato mzima wa uombaji wa chuo.
Mwanafunzi hupewa nafasi tano za kufanya udahili kutokana na fani azitakazo ,ambazo hapa unatakiwa uzipange fani hizo katika mpangilio wa priority yako.Mambo ya kuzingatia :-
I. Hakikisha ile fani ya mwanzo kabisa uipendayo katika chuo utakacho unaiweka hapa,
Mara nyingi ikiwa matokeo yako yanaruhusu katika chuo hicho kwa kuzingatia competition ilokuwepo na idadi ya wanafunzi watanaotakiwa basi inakua asilimia kubwa kukipata.
Ø Hakikisha hapa usiweke chuo ambacho kwa matokeo yako na vigezo vitakiwavyo una uhakika wa kukosa,kua makini sana katika sehemu hii.
II. Baada ya kuchagua fani ya kwanza,basi utachagua fani na chuo katika sehemu nne zilizobaki kwa kuzingatia priority yako,vigezo vya chuo na matokeo yako.
III. Nashauri ,kutokana na matokeo yako husika jaribu sana kuangalia competition ya chuo,idadi ya wanafunzi wanavohitajika na vigezo ,jaribu kuepuka kuomba chuo ambacho una uhakika hupati mfano mzuri ,kuna wimbi la wanafunzi wa PCB ambao hutaka kusomea udaktar i(medicine) katika chuo cha MUHIMBILI,hapo uwe makini sana kwani chuo hicho kwa udaktari wanachkua division one tena iliyochangamka….
IV. Selection mara nyingi wanaangalia kigezo cha,cut off point, matokeo na priority hivyo usishangae wewe na mwenzako matokeo sawa mkaomba kozi sawa lkn mpangilio tafauti lakin mmoja akapata kuchaguliwa mmoja akakosa kuchaguliwa katika raund ya kwanza,katika hili naendelea kusisitiza kuhusu ushauri kwa wenye uzoefu wa kufanya application hizo.
Angalizo: kua na minimum entry requirements katika chuo husika c sababu ya lazima kupata chuo .
Kuna factors nyingi ambazo zinachangia kama competition ya waombaji,idadi ya wanafunzi wanaohitajika katika kila fani, priority arrangements etc.
3. KUA TAYARI KUSOMA KATIKA FANI NA CHUO CHOCHOTE AMBACHO UTAKIOMBA
Kabla ya kuomba nafasi hizo tano basi ujikubalishe kua katika nafasi hizo popote utakapochaguliwa utasoma.Katika nukta hii natilia umuhim wa kua tayari kusoma popote utakapopangiwa kwani mchakato wa kudahili ni mrefu sana ambao unazingatia vigezo tafauti,hivyo unaweza kuchaguliwa nafasi hata ya tano uliyoomba,hivyo kwa kuepusha usumbufu wa baadae hakikisha unajitathimini vizuri kwanza katika selection yako.
4) KUCHAGUA CHUO AMBACHO UNAWEZA KUKILIPIA GHARAMA ZAKE ZA ADA BAADA YA KUPATA ASILIMIA YA MKOPO KUTOKA BODI YA MKOPO
Vyuo vipo vya serekali na private ,mara nyingi vyuo vya serekali ada ya chuo ni ndogo kulinganisha na private.
Hivyo nashauri,kwanza uangalie chuo unachotaka kukiomba ada yake,na asilimia ya mkopo ambao bodi wanakupatia,hivyo utapata kujitathmini na familia yako kua unaweza kulipia asilimia iliobaki au laa.
Hapa napo panahitaji umakini mkubwa ,kwani kuna wimbi la wanafunzi kila mwaka wanapata chuo lakini wanagundua ada ya chuo kikubwa sana ambacho hawawezi kukimudu hivyo wanaamua kuhairisha mwaka kuomba tena vyuo vyengine kwa mwaka mwengine.
5) Kuzingatia soko la ajira
Kama tujuavyo tunasoma lakini malengo yetu at the end of the day ni kupata ajira na si kumaliza na mavyeti na kubaki nayo nyumbani.Binafsi mimi si mtaalamu sana katika sehemu hii hivyo ninachoweza kukwambia nakuachia nukta hii uitafute kwa washauri wako na kwa watu wako wakaribu.
Kwa kweli yapo mengi sana ya kuzingatia lakin mengine utapatiwa na washauri wako ,lakini ningependa nigeuze upande wa pili wa shilingi ni nizungumzie kwa ufupi sana mambo ambayo yanaweza kujitokeza ukikosa umakini katika mchakato huu.
I. Kukosa nafasi zote tano ulizoziomba.
Matokeo yanaweza kutoka na kujikuta umekosa nafasi zote ulizoomba na hivo kutakiwa kufanya tena application katika raund nyengne,mwaka jana wanafunzi walifanya selection mpaka raund sita.
II. Kupata fani mbovu ambayo hukuitegemea kabisa.
III. Kughairisha mwaka baada ya kutoridhishwa na mchakato wa chuo ulichopata au fani uliopangiwa
IV. Kukosa chuo moja kwa moja.
Naomba nisikuchoshe kwa kukujazia mambo mingi sana katika Makala hii ,naomba uzingatie vizuri maelezo niliyoyatoa huo ni ushauri wangu tu kutokana na experience niliyoipata. Nimeandika Makala hii kwa kuona ipo haja ya kuwashauri wenzangu kua na tahadhari kwani waswahili husema “KINGA NI BORA KULIKO TIBA’’
Brought to you By DR FOC
PREP BY MASATU.
Comments
Post a Comment