Skip to main content

HOSPITALI KUBWA YA KUTIBU MAGONJWA YA KANSA


MWEKEZAJI MZAWA AAMUA KUWEKEZA KAGERA KWA KUJENGA HOSPITALI KUBWA YA KUTIBU MAGONJWA YA KANSA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA
Mkoa wa Kagera kupiga hatua kubwa kimaendeleo baada ya kujitokeza mwekezaji mzalendo ambaye ni Mshauri Mkuu wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Company Ltd ya Jijini Dar es Salaam Bwana James Rugemalila kuanza mchakato wa kujenga kituo kikubwa (hospitali) ya magonjwa ya matibabu ya Kansa katika Manispaa ya Bukoba.
Bw. James Rugemalila akiambatana na ujumbe mzito na wataalamu wa afya kutoka nchi mbalimbali alifika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 10/07/2015 na kuongea na Katibu Tawala mkoa Bw. Nassor Mnambila ambaye alimhakikishia juu ya kupata ardhi wanayohitaji na kuwa serikali ya mkoa itawaunga mkono katika hatua zote za kupatikana kwa kituo hicho.
Aidha Bw. Rugemalila na ujumbe wake walifika Manispaa ya Bukoba na kuongea na Kaimu Mkurugenzi Bw. Lukiko Chibunu ambaye pia aliwahakikishia kuwa ardhi ipo na tayari wameitenga kwa ajili ya uwekezaji huo kama walivyoombwa na Bw. Rugemalila na walidhuru eneo husika Mtaa wa Makongo karibu na Ziwa Victoria.
Ujumbe huo ulilidhishwa na eneo husika pia Bw. Rugemalila aliambatana na Profesa Anthony Pais Mkuu wa Idara ya Upasuaji kutoka Bangalore India ambaye alisema Tanzania na Mkoa wa Kagera ni muhimu kuwa na kituo hicho kutokana na takwimu za Shirika la Afya ulimwenguni (WHO).
Profesa Pais alisema kuwa wagonjwa wa kansa 35000 wanatambuliwa kila mwaka duniani na asilimia 90% ya wagonjwa wanatoka duniani kote na wagonjwa 3000 wanatoka Tanzania kila mwaka na hupelekwa nje ya nchi kutibiwa ambapo baada ya kituo hicho kujengwa itakuwa fursa kwa watanzania kupata matibabu hapa hapa nchini na mkoani Kagera.
Vilevile Profesa Pais alisema kuwa Kampuni ya VIP Engenering and Marketing Ltd iliamua kujenga kituo hicho mkoani Kagera kwasababu walipoonyeshwa eneo la Makongo katika Manispaa ya Bukoba walipendezwa nalo sana pia mkoa wa Kagera umepakana na nchi zote za Afrika Mashariki ambapo ni moja wapo ya fursa katika uwekezaji.
Naye Bw. Anic Kashasha Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano katika Kampuni ya VIP Engineering Ltd alisema kuwa kituo hicho mara baada ya kukamilika kitajulikana kwa jina la (RUTAKWABYERA CANCER HEALTH CENTER) na kitakuwa na hadhi zote za hali ya juu mpaka kawaida ili kutoa fursa kwa wananchi wote kupata huduma stahili.
Kituo hicho kwa kuanzia kitajengwa na kuanza na vitanda 100 na mara baada ya kukamilika kitakuwa na vitanda 500 pia zitajengwa hosteli za wananchi ambao watakuwa wanawaleta wagonjwa wao kupata mahala pakujihifadhi. Kitaitwa kituo badala ya hospitali kwani kitakuwa kinaendesha uchunguzi, ugunduzi, na kutoa tiba na elimu juu ya ugonjwa wa Kansa.
Kituo cha Rutakwabyera kinatarajiwa kujengwa ndani ya miaka mitatu kuanzia sasa na gharama za mradi mzima zitajulikana mara baada ya ujenzi kuanza rasmi. Mkoa wa Kagera unazo Nyanja nyingi sana za uwekezaji wazawa na wawekezaji mbalimbali mnakaribishwa kuwekeza Kagera.

Comments

Popular posts from this blog

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Medical gamble that saved a little boy’s life

  The 18-month old boy was rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) in Dar es Salaam where he was admitted. But his condition soon deteriorated into acute kidney failure. A dark cloud hovered over the family. The country’s biggest referral hospital has for years been infamous for being too ill-equipped to save those dying from such conditions. To read the whole story click here

Haya ndiyo madhara ya Kutumia earphones

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo. Akizungumza na FICHUO TZ, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’. “Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka. Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo. Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya sa...