WANANCHI WA KIJIJI CHA ILININDA WILAYANI LUDEWA WACHANGISHANA PESA MIFUKONI MWAO ILI KUKARABATI BARABARA
MTU KWAO/ Eagle Eyes

WANANCHI WA KIJIJI CHA ILININDA WILAYANI LUDEWA WACHANGISHANA PESA MIFUKONI MWAO ILI KUKARABATI BARABARA,
Na Maiko Luoga Ludewa,
Barabara ya Kutoka Kijiji cha ilawa Hadi Ilininda wilayani Ludewa imedumu kwa Muda mrefu ikiwa mbovu bila matengenezo Hatimaye Wananchi Wa Kijiji cha Ilininda kwakushirikiana na Wadau mbalimbali ndani ya Kata ya Madilu Wilayani Ludewa katika Mkoa Wa Njombe wameamua Kuingia Mifukoni mwao na Kuchangishana Pesa kwa Umoja wao ili kuikarabati barabara hiyo Bila kuisubiri Serikali.
Wakizungumza na Mwandishi wetu wananchi Wa Kijiji cha Ilininda wamesema Baada ya Kuona barabara yao Ipo katika hali mbaya wameweza kushirikiana na Uongozi Wa NGO ya IDEFO hadi kuchangia kiasi cha Sh. 15 million Ambazo tayari zimetumika Kulipia mafuta Kwa mtu aliyewasaidia kupata Mashine na Uchimbaji Wa Barabara hiyo unaendelea Huku wakiiomba Serikali kuwasaidia Pesa kwaajili ya Kuendelea Kuikarabati barabara hiyo waliyoamua kuichimba kwa Nguvu zao wenyewe.
Mh. John Mkolwe ni Diwani Wa Kata ya Madilu Amesema kuwa Mbunge Wa jimbo la Ludewa Mh. Deo Ngalawa amewaunga mkono wananchi kwakutoa kias cha sh. Lakitano Huku akieleza mgawanyo Wa Mchango kwa wananchi kwakusema wananchi Wa kipato cha kawaida wanachangia kias cha Sh. 20,000 na kuendelea na wale wenye kipato cha juu zaidi wanachangia kias cha Sh. Lakimoja na kuendelea Pia amesema wamemuandikia Barua mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Ili kuomba msaada zaidi lakini barua hiyo bado haijajibiwa.
Kutoka katika kijiji cha Ilawa hadi Ilininda wilayani Ludewa kunajumla ya Klomita 14 ambapo kwakutumia Pesa hiyo Wamefanikisha kuchimba jumla ya Klomita 10 na kazi inaendelea Huku Kaimu Katibu Wa (IDEFO) bw. Deograsias Mgina Akisema kuwa Bado wanakabiliwa na Changamoto ya PESA zaidi kwaajili ya Kuweka kifusi na kushindilia Barabara hiyo ili iweze kupitika angalau kwa Mda mrefu zaidi.
Uongozi huo Wa Kata ya Madilu kwakushirikiana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanawaomba Wafadhiri, Taasisi mbalimbali na wadau tofauti kuwasaidia Ili kuweza kukamilisha Ukarabati Wa barabara hiyo ambayo inafaida kubwa kwa wananchi Ambao ni wakulima na wafugaji Wenye kipato cha chini zaidi kiuchumi kwakuwa kwakufanya hivyo nikuwainua wanainchi hao

Comments
Post a Comment