Rwanda imeanza kutekeleza uamuzi wa kuongeza ushuru unaotozwa nguo za mitumba zinazoagizwa kutoka nje.
Uamuzi
huo ulichukuliwa na nchi za jumuiya ya afrika mashariki japo baadhi ya
nchi zilijipatia muda ili kujitayarisha zaidi kuingia katika mfumo huo
mpya wa kutumia nguo zinazotengenezwa na viwanda vya nguo vya ndani.Viongozi wa Rwanda wamekuwa katika kampeni kabambe ya kutaka wananchi kutumia bidhaa zinazotengezwa nyumbani, licha ya kwamba nchi hiyo ina kiwanda kimoja tu cha kutengeneza nguo.
Kulingana na serikali,nguo za mitumba zimeanza kutozwa ushuru wa dollar 2,5 toka dollar 0,5 kwa kilogramu moja ilhali ushuru kwa viatu vya mitumba umepanda toka dollar 0,2 hadi dollar 5 za Marekani.
BBC swahili
Comments
Post a Comment