Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2016

FAIDA ZA PAPAI KIAFYA

Papai husaidia kuyeyusha chakula mwilini kutokana na kuwa na kimeng'enya kiitwacho 'papain'. Tunda hili pia lina vitamin A na C (antioxidants). Mbali na faida hizo kwa mwili wa binadamu tunda hilo pia ni tiba kwa magonjwa mbalimbali. Mathalani, mbegu za papai hutibu kuharisha (dysentery) na minyoo kwenye njia ya mfumo wa chakula (gastrointestinal tract). Pia mizizi ya papai hutibu gono (gonorrhea). Kadhalika watu wanaosumbuliwa na maumivu ya viungo (Arthritis) na magonjwa au matatizo mengine kama mzio (allergy) asthma, hypertension, maumivu ya jino, na watu wenye tatizo la kupatwa na wasiwasi (chronic anxiety), tatizo la kinga ya mwili kuwa ndogo (low immunity), mwili kukosa nguvu, na uchovu (chronic fatigue) wanashauriwa kula papai kila siku au mara kwa mara. Kwa maneno rahisi watu wenye matatizo hayo walifanye papai kuwa rafiki yao wa karibu. Wanashauriwa kula papai asubuhi kabla ya kula chakula chochote, au watumie kijiko kidogo cha unga wa mbegu za pap...

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE

  Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na umeng’enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng’enyaji huo ni kinywa, umio/esofagasi (ujia wa msuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo), mfuko wa tumbo, ini, mfuko wa nyongo, duodenamu (sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo inayoanzia katika pilorasi ya tumbo). Nyingine ni iliamu (utumbo mdogo kati ya jejunamu na sikamu), kongosho, utumbo mpana na rektamu (sehemu ya mwishoni ya utumbo mkubwa yenye urefu wa sentimeta 13, rektamu huanzia mwishoni mwa koloni ya sigmoidi na kuishia mwanzoni mwa unyeo). Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng’enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama ‘Peptic Ulcers’. Vidonda vya mfumo wa umeng’anyaji chakula vikiw...

UHODARI, UNGANGARI NA USHUJAA WA TUNDU LISSU BUNGENI

Download Video as MP4

AY EL CHAPO Official Video1

Download Video as MP4

Bruno Alex... Dunia ya Leo

Download Video as MP4

Mindset mc ft Bode & Geof Master MATEKA

Download Video as MP4

Jinsi ya kupata mtoto jinsia unayotaka

JINSI YA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA Habari za wakati huu ndugu yangu mpendwa na mfuatiliaji mzuri wa Makala zangu za afya kupitia page yangu iitwayo Gurti health consultant. Kipindi cha nyuma alikuwa analalamikiwa mama kwa kuzaa watoto wa kike tupu au wakiume tupu pasipo kujua anayeamua jinsia ya mtoto ni mwanaume nashukuru Mungu sasa hivi jamii imeanza kutambua hilo MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE? Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X na Y za mwanaume Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto SIFA ZA CHROMOSOMES Y 1.Zina spidi  kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe  zitawahi kwend...

Lionel Messi arejea timu ya taifa ya Argentina baada ya kutafakari

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Nahodha  wa timu ya taifa ya Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, ametangaza kuwa atarejea katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina. August 12 2016 chama cha soka cha Argentina AFA kimetangaza Lionel Messi amebadili maamuzi yake na kuwa ataendelea kuichezea timu ya taifa ya Argentina. Messi,29,alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo Julai Mwaka huu kufuatia kukosa penati dhidi ya Chile katika fainali ya michuano ya Copa America Centenario na hivyo taifa hilo kupoteza fainali 3 mfululizo. . ‘Nimeona kuna matatizo mengi katika soka la Argentina na sitaki kuongeza zaidi, sitaki kusababisha maumivu , lengo langu ni kusaidia katika njia niwezayo’ amesema mchezaji huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 5. Nyota huyo ambaye ndiye mfungaji wa muda wote wa Argentina akiwa na magoli 55 katika mechi 113, Septemba mwaka huu atakuwepo katika kikosi cha kocha mpya Edgardo Bauza kitacho...

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito). Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito. Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni. Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, ina...

Wafahamu wagombea wa nafasi mbalimbali UNSATA

Habari ndugu msomaji , ni siku chache kabla ya uchaguzi wa UNISATA kufanyika.  Baadhi ya wadau wameendelea kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali ktk chama. Kwa mujibu wa m/kiti wa tume ya uchaguzi hawa ndio wagombea wa nafasi ya mwenye kiti ALDOPH ITUGA HELMAN MBIRO HUSEIN BAHANZIKA wote ni BscN2 Orodha ya wagombea wa nafasi nyingine itakujia iv karibuni Mhariri _Dr FOC @Eagle eyes

Sigara na Madhara yake

Leo tutazungumzia madhara ya kuvuta sigara, tabia ambayo imezoeleka na watu wengi ingawa ina madhara mengi. Ili kuweza kuyajua madhara hayo kwa undani, usiondoke kando ya redio yako hadi mwisho wa kipindi hiki. Kemikali zenye madhara zilizo kwenye sigara Ufutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha kansa. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa mwaka. Mada na kemikali zilizo kwenye sigara huathiri karibu kila kiungo mwilini kuanzia seli hadi mfumo wa kulinda mwili. Kemikali zilizoko kwenye moshi wa sigara huingia katika mapafu na kuenea katika mwili mzima na kusababisha madhara makubwa kwa njia mbalimbali. Ingawa mada hizo haribifu zilizoko kwenye moshi wa sigara ni nyingi, lakini tatu ni hatari zaidi zi...

UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA NA MATIBABU YAKE.. [HYPERTENSION]

Hypertension ni nini? Huu ni ugonjwa ambao hugunduliwa pale presha ya damu inapokua juu sana kupita kiwango chake cha kawaida. Kawaida damu inasukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili lakini nguvu inayotumika kusukuma damu hiyo  kutoka moyoni kwenda sehemu zote za mwili na ile ambayo inakuwepo kwenye mishipa ya damu wakati damu inapita ndio inaitwa presha ya damu. Hivyo binadamu yeyote lazima awe na presha ya damu lakini katika kiwango kinachohitajika ambacho ni 120\80mmhg mpaka 140\90mmhg zaidi ya hapo tunaita hypertension.. WALIOKO KWENYE HATARI YA KUPATA PRESHA.. umri mkubwa: wanaume wako katika hatari ya kupata presha kwenye umri wa miaka 45 na kuendelea na wanawake miaka 65 na kuendelea. Rangi ya ngozi: presha ya damu inasumbua sana watu weusi na huweza kuanza katika umri mdogo zaidi na madhara makubwa kama kupooza, moyo kusimama ghafla na kufa kwa figo hutokea kwa weusi kuliko weupe. Familia; Koo zenye wagonjwa wengi kwa presha kwani ugonjwa h...

Tambua Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara

  Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku. Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo. Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au ...

MADHARA YA KUNYWA POMBE KIPINDI CHA UJAUZITO

  Kipindi cha ujauzito kwa mama ni kipindi muhimu sana ambacho kwa wakati huu mama hatakiwi atumie kitu chochote cha kujitibu bila ushauri wa daktari kwani kinaweza kudhuru mtoto lakini pia kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama hatakiwi kunywa kileo chochote kile unachokifahamu. Sio bia, sio spirit, wala mvinyo au wine. wanawake wengi wa siku hizi hubeba mimba bila kufahamu kwamba wana mimba na huja kugundua baada ya mwezi mmoja au miwili baada ya kumshindilia mtoto pombe za kutosha.tabia hii ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto kama ifuatavyo... 1. Mtoto kua na umbo la ajabu; mtoto huweza kuzaliwa na kichwa kidogo, uso kama bapa na macho madogo sana. dalili hizi huweza kuanza kuonekana katika umri wa miaka 2 na mara nyingi mtoto hua tofauti na wenzake. 2. Kuchelewa kukua; pombe huingilia mfumo wa ukuaji na kumchelewesha mtoto kufanya baadhi ya mambo kama kutambaa, kutembea, kuongea na kadhalika. ukimuangalia mtoto mwenye umri kama huo huo ataone...

Wanafunzi Vyuo Vikuu ‘wanakula nyasi?’

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika mgomo LEO ni siku ya tatu mfululizo, tangu wanafunzi wa vyuo vikuu kote nchini kuanza mafunzo kwa vitendo (practical trainings) bila Serikali kuwapatia fedha za kujikimu ikiwemo na nauli ya kuwawezesha kufika katika vituo vyao, anaandika Charles William. Kitendo hiki ni kinyume na mkataba baina ya wanafunzi hao na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu hapa nchini (HESLB) lakini pia ni kinyume na ahadi ya serikali iliyotolewa wiki mbili zilizopita kuwa wanafunzi hao wangepewa fedha za kujikimu kwaajili ya mafunzo kwa vitendo kabla ya 8 Agosti mwaka huu. Katika mkutano na vyombo vya habari, wiki mbili zilizopita Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alidai kuwa serikali imeshindwa kuwapa wanafunzi fedha za mafunzo kwa vitendo kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi hewa na kwamba imesogeza mbele kuanza kwa zoezi hilo la kitaaluma kutoka 25 Julai mwaka huu mpaka 08 Agost...

FAHAMU KUHUSU KIFUA KIKUU (TUBERCULOSIS,TB)

MTU KWAO BLOG @#Eagle eyes Kifua kikuu ni ugonjwa unaosabishwa vimelea vidogo aina ya bakteria viitwavyo #Microbacteria_tuberculosis. Ugonjwa wa kifua kikuu unaenezwa kwa njia ya hewa kutoka katika mtu ambaye anaugua na hajaanza matibabu, mtu huyu akipiga chafya, kukohoa au kutema makohozi ovyo anaweza kuambukiza watu wengine. Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, pia kinaweza kuathiri sehemu yeyote ile nyingine ya mwili ikiwemo mifupa, tumbo na mgongo. VITU VINAVYOHATARISHA MTU KUUMWA KIFUA KIKUU(TB) Zaidi ya theluthi moja ya watu duiniani wana maambukizi ya TB lakini hawana dalili za kifua kikuu, asilimia 10 tu ndio huja kupata ugonjwa wa kifua kikuu. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili huwa imara na kuzuia vijidudu vya TB kuzaliana na kushambulia mwili. Vitu vifuatavyo huchangia kwa namna moja au nyingine kutokea kwa kifua kikuu kwa mtu asiye na maambukizi:     *UKIMWI/VVU    * Upungufu wa kinga mwilini kutokana na dawa au magonjwa mengine ukiac...

What are hemorrhoids?

MTU KWAO BLOG/ Eagle Eyes Highlights Some women will develop hemorrhoids during pregnancy. Hemorrhoids may clear up in a few days without treatment, or they may require treatment in your doctor’s office. Dietary changes can help treat and prevent hemorrhoids. Hemorrhoids are swollen veins around your anus or lower rectum. Hemorrhoids can be internal or external. Internal hemorrhoids are inside of the rectum. External hemorrhoids are outside of the anal opening. Hemorrhoids can sometimes be painful or itchy. They can also bleed during bowel movements. Hemorrhoids are very common. Seventy-five percent of people will have hemorrhoids at some point. Hemorrhoids are more common in people between the ages of 45 and 65. Advertisemen How long do hemorrhoid symptoms last? If your hemorrhoids are small, your symptoms may clear up in a few days without treatment. You may also need to make simple diet and lifestyle changes. Some internal hemorrhoids become so enlarged that they stick o...

UTI NA TIBA YAKE.

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Maambukizi Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya magonjwa ambayo hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake. Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema. Wataalamu wa afya wanasema UTI husababishwa na vimelea ambao huingia kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la kudumu. Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria walio wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli). Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini husafiri kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha maambukizi katika kibofu na figo. UTI inavyoenea...

SUPU YA PWEZA NA NGUVU ZA KIUME

Utafiti: Wataalamu/wanasayansi wa Ndani kutokea Muhimbili, na wa Kimataifa, wamethibitisha kuwa Supu ya Pweza ni Mujarab kwa kuongeza Nguvu za kiume. Wadai uwezo wake ni 'tahmimu' ukilinganisha na Madawa mengine ya Kemikali. Neno moja kuihusu Supu hii!!!

DAKTARI FEKI AFANYA KAZI KWA MIAKA 10 KAMA DAKTARI BINGWA

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Jamaa huyu amefanya kazi kama Daktari Bingwa kwenye Hospitali moja nchini Nigeria kwa Miaka 10 bila kugundulika. Kosa lake kubwa ilikuwa ni kupiga picha akiwa ameshika kiungo cha binadamu na kutupia kwenye mtandao wake wa kijamii ndipo wanoko walipoanza kumfuatilia na kugundua kuwa sio daktari.

Nafasi ya kazi kwa Daktari wa Meno

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes  AL ABBAS DENTAL CLINIC INATANGAZA NAFASI YA KAZI KWA DAKTARI WA MENO   (DENTAL THERAPIST)          MUOMBAJI AAMBATANISHE VITU VIFUATAVYO                        1. BARUA YA KUOMBA KAZI, CV YAKE.                 2. CHETI CHA KUMALIZA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA                 3.CHETI CHA KUMALIZA KOZI KATIKA CHUO HUSIKA.                             4.CHETI CHA KUZALIWA,                                      TUMA MAOMBI YAKO KWA EMAIL IFUATAYO       alabbasdentaclinic@gmail.com  au mubason@gmail.com SIMU 0767291030 /0677010050            ...

IMANI POTOFU KUHUSU AFYA YA KINYWA NA MENO

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes 1.POTOFU:  Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno UKWELI:  Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika, suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu kunaweza kupelekea kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika. Kupiga mswaki marambili, taratibu na kwa njia sahihi ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya 2.POTOFU:  Huna haja ya kumuona tabibu wamenokama hujaona au kuhisi una tatizo la meno. UKWELI:  Kila mtu anatakiwa kumuona tabibu wa meno angalau mara mbili kwa mwaka bila kujali meno yake yanaonekana vizuri au imara kiasi gani. Si meno yote yanayo onekana mazuri na imara ni mazima, mengine yanaweza kuwa yameoza katikamaeneo usiyoweza ona kama chini ya fizi na kwenye mizizi, si hivyo tu hata uoto mpya(neoplasm)uweza kugundulika mapema kabla ya kufanya uaribifu mkubwa kama utachunguzwa na wataalamu. Kumbuka pia ...

KULEGEA KWA MISULI YA UKE (VAGINAL PROLAPSE)

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes Tatizi hili huwatokea zaidi wanawake walio kaika umri mkubwa ingawa pia linaweza kutokea katika umri mdogo.Tunapozungumzia kulegea kwa misuli ya uke hapa kuna tofauti kidogo na kutanuka kwa misuli hiyo.Tukizungumzia kulegea ina maana misuli ya ukeni inashindwa kubcana na kuachia njia.Hapa misuli inayoachia njia inapolegea hata ukichuchumaa uhisi nyama zimejaa ukeni. Chanzo cha tatizo Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike,kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV,Magonjwa ya zinaa haswa kawende pia huchangia. Kulegea kwa misuli ya uke kutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu,mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili,kulegea kutokana n...

IJUE HOMA YA MANJANO HAPA

MTU KWAO BLOG / Eagle Eyes CHANZO, ATHARI  , KINGA   NA  TIBA  YA  UGONJWA  WA  MANJANO. Ugonjwa    wa  Manjano    ambao  hufahamika  kitaalamu  kama  HEPATITIS  B  ni  hatari  sana  na  umesababisha  vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote.    Kwa  mujibu  wa  ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  ( W.H.O )   kuna  zaidi  ya  wau  Milioni  350  duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu  hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa  kila  mwaka  kwa  ugonjwa  wa  Manjano. CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hep...